Shughuli ya kusahihisha mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, KCSE inatarajiwa kukamilika Alhamisi ,Disemba 12
Walimu waliokuwa wakisahihisha mtihani huo wataondoka vituoni Ijumaa, Disemba 13 kuelekea makwao.
Waziri wa Elimu George Magoha anatarajiwa kutangaza matokeo ya mtihani huo siku ya Ijumaa, Disemba 20.
Habari Nyingine: Gavana Sonko aachiliwa huru kwa damana ya 30M, haruhusiwi kuingia ofisini
Habari Nyingine: Nairobi yawika ndani ya Afrika kama mji bora
Shughuli ya usahihishaji mtihani huo ilianza Novemba 28, siku moja baada ya watahiniwa kumaliza kuufanya mtihani.
Mtihani huo ulianza Novemba 24, na kukamilika Novemba 27, huku visa 21 vya udanganyifu vikiripotiwa.
Magoha alisema zaidi ya shule 300 ziliripotiwa kuhusika katika wizi wa mtihani ila ziliwekwa chini ya ulinzi mkali.
Read: ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4Z1hJJmqqGtl53CrbWMsphmo6Worqm1x6KqoZldosGqtMCnoGavkWK4qsDAop2aZaeWeqyv0p5kpK2blrqquMikmGaZnJ2urrXSopuiq5Wir6J5kGtloaydoQ%3D%3D